TEGEMEO LETU ni Elimu
SAUTI YA WANAZUONI
Tuesday, August 25, 2015
MUENDELEZO WA KITABU CHA SABABU MBADALA ZA UMASKINI WA TANZANIA - SURA YA PILI
SURA YA PILI
KUUA NGUVU ZA ASILI ZA MAKABILA YETU.
Kama nilivyosema katika dibaji ya kitabu hiki, maandishi yangu hayazingatii sana utafiti wala utaalamu wa uandishi na wala rejea zozote, ni mawazo binafsi ambayo wengine wanaweza kukubali au kukataa ni katika mitazamo tuu.
Tukijaribu kurudi nyuma katika maisha ya jamii nyingi za waafrika hasa hapa Tanzania, tunakutana na tamaduni mbalimbali za makabila mbalimbali zilizolenga katika kuheshimiana, kushirikiana, kupendana na kulindana. Makabila haya yalikuwa na taratibu mbalimbali zinazosimamia maendeleo yao ya kijamii, mifumo ya uongozi, na namna mbalimbali ya kukabiliana na majanga kama ya njaa, moto, magonjwa n.k.
Kila kabila kwa asili yake lilikuwa na namna lilivyomuandaa mtoto hadi ujana ili akubalike kuwa mwanajamii wa kawaida. Alipimwa kwa mambo mengi ya ushujaa, uchapa kazi, ubunifu, unadhifu, uadilifu na weledi katika utendaji wa shughuli za maendeleo. Jamii ikimpata kijana kama huyu itamkabidhi mke ambaye naye atachaguliwa kulingana na vigezo hivyo. Changamoto kwa hiyo ni uwezo wa kila mwanajamii kuwa mzalishaji kwa kuwa jamii iliwategemea vijana hawa moja kwa moja.
Makabila kama ya Masai, Wachaga, Wasukuma, Wahaya, Wakwere, Wamakonde, Wazigua na mengine yalikuwa na namna yalivyokuwa yanaratibu ukuaji wa vijana wake hadi kuwa watu wa wazima ambao sasa wangeweza kushiriki katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kijamii katika kujitafutia maendeleo.
Leo kwa kuwa jamii pana ya Tanzania inadai imeendelea, na hapa ikumbukwe kuwa hakuna jamii ya Watanzania. Jamii hii inazaliwa kutoka katika makabila yaliyoko Tanzania chini ya mwavuli wa tamaduni na mila, desturi na maadili ya makabila husika, tumekuwa na dhana inayoitwa kupambana na ukabila.
Dhana hii inatiliwa nguvu na ukweli kuwa mwanadamu anapenda kuhusiana sana na yule anayemfahamu, aliyekaribu nae na ambaye anaamini kati yao ni wamoja. Ndio maana ukiwa CCM unamuona Mwana CCM ni ndugu yako, ukiwa CHADEMA au CUF nakadhalika. Ukiwa Mwislam vivyo hivyo, na kwa makundi mbalimbali ya kijamii.
Kinachoshangaza hapa ni mikakati ambayo inawekwa mahususi katika kuangamiza kinachoitwa Ukabila. Lengo likiwa ni kutengeneza jamii moja pana inayoitwa ya Watanzania.
Katika makabila haya tumeona miundo mingi ya usimamizi wa maadili inavyosimamiwa na mila na desturi kwa watu wa makabila hayo. Je mila na desturi zitakazoisimamia Tanzania ni zipi? Ndio maana Ulaya na mabara mengine kumekuwa na mmomonyoko wa maadali kwani mdumo wa kijamii umeparaganyika.
Hajulikani baba, mama, babu, bibi, mtoto au mjukuu. Hii inatokana na wao kuua mfumo wa asili wa mahusiano ya kijamii na kuunda hiki tunachotaka ambacho ni jamii iliyoondokana na ukabila.
Kwa nini katika makundi mengine tunatengeneza lugha ya kuvumiliana na sio kwenye makabila. Kwenye dini utasikia tujenge uvumilivu, kwenye vyama vya siasa tujenge uvumilivu, kwenye kabila – tutokomeze ukabila. Je manufaa yake siku za mbeleni ni yapi?
Tujaribu hata kuangalia katika wakati tulionao. Vijana wengi wamechanganyikiwa, hawajui tena asili ya utamaduni wanaotakiwa kufuata. Leo kwa kuwa dhana ya ukabila imewaingia kama sumu hawataki kufahamu hata mila na desturi zao ambazo ndizo zingewajengea taswira ya Uafrika wao. Hawana urithi wa kijamii unaotokana na mwendelezo wa fikra zenye ushawishi wa kimwamko.
Mathalani wachaga ni wafanyabiashara lakini kwa leo vijana wao hawataweza tena kufanya biashara kama ilivyokuwa kwa wazazi wao. Wamasai kwa mfano ni wafugaji, lakini leo hawawezi tena kuendana na mfumo uliowapa nidhamu na kujambua na kuthamini kile kinachomilikiwa na jamii, ambacho ni mifugo.
Katika ufumaji mpya wa makundi haya ya kijamii, ili yaendane na mwenendo huu wa kisasa wa kuua ukabila, lazima tuwe makini kwani ndani yake tunaua teknolojia za asili, ubunifu, nidhamu, maadili, mila na desturi kama tutakavyoona katika sura ijayo, na mwisho ni kuwa na Taifa linalojiita moja lakini likiwa limeparaganyika kama nchi za Ulaya zilivyo leo.
Kuparaganyika huku tuna maana gani? Ni pale ambapo kama jamii, hatuna tena mfumo wa malezi ya kijamii kulingana na mila na desturi, bali tumebaki tunatengeneza taasisi za mpito za malezi kama vile Jeshi la Kujenga Taifa na nyingine. Je tuulizane, JKT imeweza kweli kuwajengea maadili wale walio waliojiunga nalo? Mfano viongozi, wana maadili ya uongozi? Wanafahamu dhima ya utu na watu hivyo kutumikia jamii kikamilifu? au kwa mfumo wa kijamii kati ya Baba, Mama, Mtoto, Babu, Bibi, Mjomba, Shangazi, Binamu na jamii yote, taasisi hizi zina uwezo kuwajengea taswira watoto, na vijana kutambua wajibu wao?? Tutafakari kwa kina kabla ya kuingia Sura nyingine ya Kitabu hiki.
Saturday, June 27, 2015
UMASKINI WA TANZANIA: SABABU MBADALA ZA UMASKINI WETU
DIBAJI
Kumekuwa na maelezo
na sababu nyingi zinazotolewa kuhusu umaskini wa jamii ya Tanzania. Wako
wanaosema kukosekana kwa uwekezaji ni chanzo kikubwa cha uchumi wetu kuyumba.
Lakini katika
kuvutia uwekezaji huo, lazima tujiulize, je fursa zinazojitokeza za kiuchumi
zina uwezo wa kubadilisha uchumi wetu kutoka katika hali duni?
Changamoto nyingine
inayosemwa ni juu ya Teknolojia. Je teknolojia hii hasa hasa ya kutoka nje inasaidia
uchumi wetu kukua? Na kama ni hivyo ukuaji wake una changamoto gani?
Changamoto za elimu,
mathalani ni elimu gani ambayo inatolewa na ina manufaa gani kwa umma?
Lakini pia,
hatudhani kuwa kuna matatizo au sababu nyingine ambazo zinachangia suala zima
la umaskini wa Tanzania na kuwa ni sababu hizi tunaishi nazo na ni sehemu ya
kawaida ya maisha ya watu?
Kupitia kitabu hiki
nitajitahidi kuainisha sababu mbadala za Tanzania na Watanzania kuwa maskini
katika nchi yenye utajiri mwingi wa mali asili kuliko nchi nyingi
zilizoendelea.
SURA YA KWANZA
MATUMIZI YA LUGHA
ISIYO YA ASILI KWA MTANZANIA -
KISWAHILI
Kiswahili ni lugha
sasa ya kimataifa. Ni lugha ambayo wengi hatuwezi tena kukataa kuwa ina mashiko
kijamii na kimataifa na mikakati ni kuifanya iwe lugha kuu hapa Afrika. Wazo
kama hili ni jema sana. Litaifanya Afrika iwe na lugha yake pekee ambayo
imetokana na eneo la Afrika na ambayo imeweza kutumiwa na jamii pana.
Nchi ya Tanzania ina
uzoefu mkubwa wa matumizi ya Kiswahili hasa kutokana na kuwa na pwani kubwa ya
Afrika Mashariki, na inavyosemekana ndiyo imekuwa kiungo cha kuleta umoja na
amani iliyopo leo. Wakati wa kupambana na wakoloni inasemwa Kiswahili kilikuwa nguzo
moja wapo ya kuwaunganisha Watanganyika wakati huo. Na katika Mapinduzi ya
Zanzibar, Kiswahili pia kilitumika kuwaunganisha Wazanzibar.
Kiswahili kina mengi
sana ya sifa kama ilivyo kwa uwepo wa lugha nyingine duniani. Kusudi langu la
kuandika kitabu hiki sio kueleza yale ambayo tayari yamekuwa yakielezwa kuhusu
Kiswahili na umuhimu wake katika maisha yetu ya kila siku.
Bali, ni kuona namna
lugha inavyoweza kuwa na athari pana katika maisha ya kila siku ya jamii
inayoitumia. Kiswahili kinabeba dhana ya uswahili. Uswahili unabebwa na dhima
ya Mswahili. Mswahili ni nani?
Tukijaribu kurudi
nyuma katika maisha ya makabila mbalimbali na hasa yale kwa namna moja au
nyingine yalitoa mchango katika kukitengeneza Kiswahili (makabila ya pwani)
ambayo yalipata bahati kukutana katika shughuli mbalimbali za kijamii, na
Waarabu tunapata kizazi kipya hiki cha Mswahili.
Kiswahili kimsingi
kimechangiwa kwa karibu sana na Waarabu, Wahindi na makabila mengi ya Pwani ya Afrika
Mashariki. Makabila yetu ya pwani, Waarabu na Wahindi hawa kimsingi walijua
lugha zao za asili, yaani lugha za makabila yao, kwa Waarabu - Kiarabu na kwa
Wahindi - Kihindi. Wote hawa walishirikiana katika biashara, kuoleana na
kadhalika. Katika kutafuta kuwasiliana, ndipo Kiswahili kikazaliwa. Kimeendelea kupanuka kutokana na mwingiliano
wa jamii nyingine za makabila na nchi nyingine ijapokuwa hakijapoteza ile dhima
yake ya uswahili.
Jamii iliyozaliwa hapa ilitengeneza
ustaarabu wa namna yao ya kuishi na kufanya shughuli zao za maendeleo. Kama
ilivyokuwa Uarabuni kuna mafuta, na Pwani kuna mazao ya samaki yaani kuvua, pia
pwani kuna mazao ya muda mrefu kama minazi, mikorosho na miembe, mwingiliano
huu ukaleta ile dhana pwani shughuli nyingi zinasimamiwa na “uasilia” wa
MAZINGIRA (Waarabu - Mafuta).
Je ni aina gani ya biashara au shughuli gani
walizokuwa wanafanya? Na baada shughuli za uzalishaji mali ambazo kimsingi ni uchimbaji
mafuta kwa Waarabu (na hapa hufanyika na makampuni sio mtu binafsi na kutokana
na mazingira hakuna uzalishaji wa moja kwa moja wa shughuli nyingine –
UKAME wa jangwa) na kuvua kwa makabila
ya pwani, basi walijipumzisha huku wakicheza michezo mbalimbali. Je mfumo wa
michezo yao ulikuwa au ukoje mpaka leo?
Utamaduni uliozaliwa hapa ni ule wa
kuitegemea asili (nature) ikupatie kile unachokitafuta. Kwa kuwa uwepo wa
mafuta ni wa muda mrefu, vivyo hivyo kwa samaki katika bahari na maziwa,
Mswahili aliyetengenezwa hapa alijikuta akiwa mtu mwenye kusubiri, kujenga
matumaini ya kujua maisha yanaendelea hakuna tatizo. Utamaduni ambao jamii
haina uwajibikaji wa moja kwa moja.
Alilima mazao yanayotoa mazao kwa muda mrefu
kama minazi, korosho, maembe na kadhalika.
Hakuwa tayari kufanya shughuli ambayo kwake
ni shulba na ambazo hata baada ya kuja kwa wazungu walipoambiwa wazifanye
waliona adhabu kama kilimo cha katani na mazao mengine, utengenezaji wa miundo
mbinu n.k.
Ndipo katika Kiswahili tunakutana na neno pole
kwa kazi! Kwa sababu kazi haikuchukuliwa kama kitu chema, ni cha kuudhi na
kinachofanywa na yule mwenye matatizo makubwa katika maisha yake. Asiye na
matatizo hatakiwi kufanya kazi na akionekana ni alama tosha kuwa ana shida
katika maisha yake.
Mfumo wa kufikiri kwa mtu aliyetokana na
uswahili (Kiswahili kikiwa ndiyo msafirishaji wa maadili na teknolojia), hakuashirii
msukumo wa uzalishaji katika kiwango cha juu bali kuwa mtu mwenye subira –
“Subira yavuta heri”. Je ni kweli katika maendeleo tuwe na subira? Na je heri
inatafutwaje?
Tunapozunguza leo, tukienzi Kiswahili ni
lazima tukichunguze kwa makini pamoja na kuleta umoja na amani, je vitu hivi
vimetupa manufaa gani? Ni yale yakutoona damu ikimwagika kutokana na matumizi
ya silaha?
Je mbona damu nyingi zaidi inapotea kutokana
na uvivu na uzembe unaofanywa na hao ambao wamekuzwa na Uswahili na Kiswahili
na sababu kuu ni mfumo wa Kiswahili katika Maisha?
Je, ni
wangapi wanashindwa kutimiza ndoto zao kwa kukumbana na Uswahili katika
utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku. Je, Uswahili unanasibishwa na nini;
sio uvivu, uzembe, majungu, wivu unatokana na wengi kutopenda kazi hivyo
kunyang’anyana kidogo kilichopo?
Je, ni kweli kuwa
watanzania wengi hawana uwezo wa kushindana katika Afrika Mashariki kutokana na
lugha ya Kiswahili au na tabia za Kiswahili na Uswahili? Je nchi nyingine jamii
zinazozungumza Kiswahili wanachukuliwaje mathalani Burundi, Rwanda, Uganda na
Kenya? Unapita sehemu fulani ya nchi unasikia “hapa ni kwa Waswahili”!!
Wanakuwa na vigezo gani?
Ndipo sasa tunafikia
suluhisho la kutafuta mfumo mwingine wa mawasiliano, usiotokana na Kiswahili,
wenye asili ya kiafrika, unaweza kutoa picha ya msukumo wa asili yetu kufanya
kazi kwa juhudi na kuwa na msukumo wa “performance”. Kuwa tunatamani kupata
maendeleo, huku mfumo wetu hauna uasilia wa kimfumo kutusukuma kufanya kazi kwa
weledi, kwa juhudi na maarifa.
Aidha, naomba
tujadiliane kwa hoja ili tuone kama haya ninayoleta kwenu yana mashiko au laa!
Na tufikie wote kuamua mustakabali wa taifa.
Tuesday, April 7, 2015
BETRI ZA SIMU ZENYE KUCHAJIWA KWA DAKIKA MOJA (1) ZAGUNDULIWA
Sayansi imepanuka na teknolojia inabadilika haraka sana. Je unaweza kuamini kuwa mateso yako ya kuchaji simu yaweza kuondolewa kwa Dakika Moja (1)? Nadhani ni jambo ambalo hatuwezi kuamini kwa haraka.
Basi kwa taarifa yako, Chuo Kikuu cha Starnford, California cha nchini Marekani kimegundua Betri yenye kuchajiwa kwa muda dakika moja. Betri hiyo inayotengenezwa kwa viasili vya "Aluminium" ina uwezo wa kuchajiwa mara 7500 tofauti na betri za sasa ambazo zimetengezwa kwa viasili vya "Alkaline" na "Lithium-ion" na zinaweza kuchajiwa kwa makisio ya mizunguko 1000.
Betri zenye viasili vya "Alkaline" na "Lithium-ion" huweza kulipuka kwa haraka ziwapo popote, mfukoni, kwenye umeme wakati wa kuchaji au wakati unatumia hivyo kuhatarisha maisha ya mtumiaji. Tofauti na betri hizi, betri hii mpya hailipuki, unaweza kuikunja au kuisokota hivyo inaweza kutumika katika vifaa vya aina mbalimbali hata kama ni vyembamba kwa kiasi gani (flexible).
Kwa mujibu wa Jarida la "Nature" lenye kuandika ugunduzi wa Kisayansi, Betri hii itakuwa ni suluhisho kubwa kwa mazingira kwani haina hatari kubwa kama zenye viasilia vya "Alkaline" na "Lithium-ion". Jarida hilo linasema betri hiyo inaweza kudumu kwa muda mrefu zaidi hivyo kuwa bora zaidi kwa watu wenye vipato vya chini.
Betri hizi zitaanza kupataikana katika matumizi ya kawaida mara baada ya makampuni ya simu kutengeneza muundo muafaka wa matumizi ya betri hii.
KWA HABARI ZA KISAYANSI, BIASHARA, UCHUMI, ELIMU, FALSAFA, MICHEZO, UTAMADUNI N.K. SOMA GAZETI LA TEGEMEO LETU au Blog hii. tegemeoletu.blogspot.com
Basi kwa taarifa yako, Chuo Kikuu cha Starnford, California cha nchini Marekani kimegundua Betri yenye kuchajiwa kwa muda dakika moja. Betri hiyo inayotengenezwa kwa viasili vya "Aluminium" ina uwezo wa kuchajiwa mara 7500 tofauti na betri za sasa ambazo zimetengezwa kwa viasili vya "Alkaline" na "Lithium-ion" na zinaweza kuchajiwa kwa makisio ya mizunguko 1000.
Betri zenye viasili vya "Alkaline" na "Lithium-ion" huweza kulipuka kwa haraka ziwapo popote, mfukoni, kwenye umeme wakati wa kuchaji au wakati unatumia hivyo kuhatarisha maisha ya mtumiaji. Tofauti na betri hizi, betri hii mpya hailipuki, unaweza kuikunja au kuisokota hivyo inaweza kutumika katika vifaa vya aina mbalimbali hata kama ni vyembamba kwa kiasi gani (flexible).
Kwa mujibu wa Jarida la "Nature" lenye kuandika ugunduzi wa Kisayansi, Betri hii itakuwa ni suluhisho kubwa kwa mazingira kwani haina hatari kubwa kama zenye viasilia vya "Alkaline" na "Lithium-ion". Jarida hilo linasema betri hiyo inaweza kudumu kwa muda mrefu zaidi hivyo kuwa bora zaidi kwa watu wenye vipato vya chini.
Betri hizi zitaanza kupataikana katika matumizi ya kawaida mara baada ya makampuni ya simu kutengeneza muundo muafaka wa matumizi ya betri hii.
KWA HABARI ZA KISAYANSI, BIASHARA, UCHUMI, ELIMU, FALSAFA, MICHEZO, UTAMADUNI N.K. SOMA GAZETI LA TEGEMEO LETU au Blog hii. tegemeoletu.blogspot.com
Sunday, March 8, 2015
NAFASI ZA SHULE
Shule ya Brain Trust Pre Primary, Secondary na High School zinatangaza nafasi za masomo kama ifuatavyo:-
1. Nafasi za Nursery (Lower, Middle na Top Class)
2. Nafasi za Primary (Darasa la Kwanza hadi la Saba)
3. Nafasi za Kidato cha Kwanza hadi Kidato cha Nne
4. Nafasi maalumu kwa Kidato cha Tatu kwa wale waliohitimu Kidato cha Nne na kushindwa kupata
sifa za kujiunga na Kidato cha Tano.
5. QT (Sekondari miaka miwili)
5. Nafasi za Pre Form Five kwa wale wanaohitaji kuanza masomo ya Kidato cha Tano mapema.
6. Nafasi za Kidato cha Tano kuanzia Julai, 2015.
Ada ni nafuu na inalipwa kwa awamu. Njoo sasa Brain Trust Schools upate elimu bora. Shule ipo
Buza Kanisani, Barabara ya Buza, Temeke, Dar es Salaam. Uliza BRAIN TRUST
Au piga simu 0755944707, 0714226080.
Njoo uchukue Fomu sasa
1. Nafasi za Nursery (Lower, Middle na Top Class)
2. Nafasi za Primary (Darasa la Kwanza hadi la Saba)
3. Nafasi za Kidato cha Kwanza hadi Kidato cha Nne
4. Nafasi maalumu kwa Kidato cha Tatu kwa wale waliohitimu Kidato cha Nne na kushindwa kupata
sifa za kujiunga na Kidato cha Tano.
5. QT (Sekondari miaka miwili)
5. Nafasi za Pre Form Five kwa wale wanaohitaji kuanza masomo ya Kidato cha Tano mapema.
6. Nafasi za Kidato cha Tano kuanzia Julai, 2015.
Ada ni nafuu na inalipwa kwa awamu. Njoo sasa Brain Trust Schools upate elimu bora. Shule ipo
Buza Kanisani, Barabara ya Buza, Temeke, Dar es Salaam. Uliza BRAIN TRUST
Au piga simu 0755944707, 0714226080.
Njoo uchukue Fomu sasa
MSINGI MATOKEO MAKUBWA SASA NI NIDHAMU
Taifa kwa sasa liko katika vuguvugu la
Matokeo Makubwa Sasa ikiwa ni msukumo wa Serikali ya Awamu ya Nne kuhakikisha
sekta zinazogusa maisha ya watu moja kwa moja mfano maji, afya, elimu,
usafirishaji na kilimo sinaangaliwa kwa jicho la pekee na Serikali.
Upande wa elimu, msukumo umewekwa
katika kuongeza udahili hasa wa wanafunzi wa sayansi ili kubabiliana na
upungufu wa wataalamu wa fani mbalimbali wa fani za sayansi.
Katika kuhakikisha hilo, jamii kupitia
asasi, mashirika ya dini, Serikali zinatakiwa kuweka msisitizo wa ujenzi wa
miundombinu yenye uwezo wa kuzalisha wahitimu wenye uwezo wa kupambana na
changamoto za kiutafiti, na kiutekelezaji katika fani hizo za sayansi
Lakini pamoja na utekelezaji wa mipango
na mikakati mingi ya kuhakikisha mafanikio yanapataikana, msingi imara katika
mafanikio hayo ni nidhamu.
Hilo limedhihirishwa na matoke ya
Kidato vidato vya Nne na Sita katika
shule zilizo chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, mathalani kwa shule zilizo
chini ya Jeshi la Kujenga Taifa; Jitegemee na Kawawa Sekondari. Matokeo ya
Shule yameonesha pamoja na kuwa na miundombinu na walimu wenye uwezo, dhana ya
nidhamu ni muhimu katika kufundisha na kujifinza.
Matokeo hayo ambayo Shule
ya Sekondari Kawawa (JKT) imefaulishwa kwa 100% na Jitegemee 97.2%
yamedhihirisha namna shule hizi zilivyodhamiria kuwa shule bora hapa nchini, na
kuwa tegemeo kwa Taifa.
Kwa upande wa Jitegemee (JKT)
Sekondari, mwanafunzi anapojiunga na shule anapitia mafunzo ya Kwata na kwa
ujumla ukakamavu. Mafunzo haya hutolewa kwa wanafunzi wapya wa Kidato cha
Kwanza na Tano na wahamiaji katika vidato vingine.
Mafunzo haya yamesaidia sasa wanafunzi kujenga utayari wa kujitunza
hasa katika utimamu wa mwili na akili, utayari wa kupokea maelekezo na maarifa katika ujifunzi, na kwa jumla
nidhamu ya kutambua wajibu wa kila mwanafunzi katika kutumia maarifa anayopata
kwa ajili yake, na jamii inayomzunguka.
Jitegemee na Kawawa sekondari zimekuwa
ni alama ya ufanisi wa Jeshi la Kujenga Taifa katika eneo la utoaji elimu bora.
Shule hizi zimekuwa na sifa ya pekee katika malezi na mafanikio ya wahitimu
wake baada ya kuhitimu masomo yao kwani wameajiriwa na kujiajiri katika
serikali kuu, sekta ya umma na binafsi.
Mfano Waheshimiwa Jerry Slaa (D)
Mstahiki Meya wa Ilala, Mhe. Lucy Mayenga Mkuu wa Wilaya, Mhe. Neema Mgaya
Mbunge; wasanii kama Marehemu Kanumba, Kajala, Temba (Mhe. Temba), Ras Pompi
Du, wacheza mpira maarufu kama Ally Mayai Tembele, Renatus Njohole (anayecheza
nje ya nchi) na wengine wengi waliohitimu Jitegemee.
Msingi wa mafanikio ni
nidhamu ambayo imesimamiwa vyema na Menejimenti ya Shule, walimu, wafanyakazi
wasio walimu, Serikali ya Wanafunzi, wanafunzi wenyewe na kwa ujumla mfumo bora
wa Jeshi la Kujenga Taifa, wa kuratibu na kusimamia utendaji na utekelezaji wa
majukumu kwa viongozi wote walio katika nafasi mbalimbali ndani ya Jeshi hilo.
Sunday, August 24, 2014
Sunday, July 13, 2014
Friday, July 4, 2014
MTANANGE WA BRASIL NA COLOMBIA
Leo ni leo katika Mtanange kati ya Timu ya Taifa za Brasil na Colombia. Hili linatokana na ukweli kuwa timu hizi ziko ukanda mmoja, na wanacheza mpira kidago unaofanana. Tofauti itakuwa katika ukweli kuwa Brasil inatakiwa kushinda ili kuwafanya watu wa Brasil ambao hivi karibuni wamekuwa katika maandamano makubwa kupinga gharama kubwa za maandalizi ya kombe hilo, angalau waendelee kuwa watulivu. Timu hizo zinategemea kutumia mifumo: Brasil 4-2-3-1 Cesar; Alves, Silva, Luiz, Marcelo; Fernandinho, Gustavo; Hulk, Oscar, Neymar; Fred. na Colombia: 4-4-2 Ospina; Zúñiga, Zapata, Yepes, Armero; Cuadrado, Aguilar, Sanchez, Rodríguez; Gutiérrez, Martínez. Huku mwamuzi akiwa Carlos Velasco Carballo kutoka Spain
WACHEZAJI WA UJERUMANI WAKUMBWA NA UGONJWA
RIO DE JANEIRO (Ap)
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Ujerumani wamekumbwa na ugonjwa kabla ya mechi yao ya Robo Fainali na timu ya Taifa Ufaransa. Akiongea na vyombo vya habari, Kocha wa timu ya Ujerumani Joachim Loew alisema "theluthi moja ya kikosi chetu wamekuwa wakilalamika kuhusu kuwashwa koo" hii inafikiriwa ni kutokana na hali ya hewa. Alisema hata mchezaji beki wa kati Mats Hummels alishindwa kicheza mechi ya kufuzu na Aljeria, lakini akawa na matumaini atacheza katika Robo Fainali na Ufaransa.
KOCHA WA BRASIL AMWALIKA MWANASAIKOLOJIA KUSAIDIA WACHEZAJI
Kocha wa Brasil Philip Scolari amemwalika Mwanasaikolojia, Regina Brandao ili asaidie Wachezaji kupambana na msongo wa mawazo unaotokana na kutakiwa kushinda mchezo wao wa Robo Fainali na timu ya Colombia. Hili linatokana na ukweli kuwa timu ya Brasil ambayo ni timu mwenyeji kucheza mbele ya mashabiki ambao lengo lao ni ushindi, ni vigumu. Akizungumza na Shirika la Habari AFP Neymar alisema hajawahi kukutana na jambo kama hili (Kombe la Dunia)na kuwa anafurahi sana. Alisema "ni sisi tu tunaocheza ndio tuna msongo wa mawazo kwa wakati wote wa pambano hivyo kupata mtaalamu wa saikolojia itatusaidia" alimaliza.
Subscribe to:
Posts (Atom)