Tuesday, April 7, 2015

BETRI ZA SIMU ZENYE KUCHAJIWA KWA DAKIKA MOJA (1) ZAGUNDULIWA

Sayansi imepanuka  na teknolojia inabadilika haraka sana. Je unaweza kuamini kuwa mateso yako ya kuchaji simu yaweza kuondolewa kwa Dakika Moja (1)? Nadhani ni jambo ambalo hatuwezi kuamini kwa haraka.

Basi kwa taarifa yako, Chuo Kikuu cha Starnford, California cha nchini Marekani kimegundua Betri yenye kuchajiwa kwa muda dakika moja. Betri hiyo inayotengenezwa kwa viasili vya "Aluminium" ina uwezo wa kuchajiwa mara 7500 tofauti na betri za sasa ambazo zimetengezwa kwa viasili vya "Alkaline" na "Lithium-ion" na zinaweza kuchajiwa kwa makisio ya mizunguko 1000.

Betri zenye viasili vya "Alkaline" na "Lithium-ion" huweza kulipuka kwa haraka ziwapo popote, mfukoni, kwenye umeme wakati wa kuchaji au wakati unatumia hivyo kuhatarisha maisha ya mtumiaji. Tofauti na betri hizi, betri hii mpya hailipuki, unaweza kuikunja au kuisokota hivyo inaweza kutumika katika vifaa vya aina mbalimbali hata kama ni vyembamba kwa kiasi gani (flexible).

Kwa mujibu wa Jarida la "Nature" lenye kuandika ugunduzi wa Kisayansi, Betri hii itakuwa ni suluhisho kubwa kwa mazingira kwani haina hatari kubwa kama zenye viasilia vya "Alkaline" na "Lithium-ion". Jarida hilo linasema betri hiyo inaweza kudumu kwa muda mrefu zaidi hivyo kuwa bora zaidi kwa watu wenye vipato vya chini.

Betri hizi zitaanza kupataikana katika matumizi ya kawaida mara baada ya makampuni ya simu kutengeneza muundo muafaka wa matumizi ya betri hii.

KWA HABARI ZA KISAYANSI, BIASHARA, UCHUMI, ELIMU, FALSAFA, MICHEZO, UTAMADUNI N.K. SOMA GAZETI LA TEGEMEO LETU au Blog hii. tegemeoletu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.