KONA YA MICHEZO NA BURUDANI


MASHINDANO YA FEASSSA YAKAMILIKA: Jiji la Dar es Salaam hususan Shule za Sekondari jijini zilikuwa ni wenyeji wa Mashindano Makubwa ya Michezo iliyokuwa inaziunganisha Shule za Skondari kutoka nchi zote za Afrika ya Mashariki yaani Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, Zanzibar na Tanzania Bara. Miongoni mwa michezo iliyofanyika ni pomoja na Mpira wa Miguu, Mpira wa Kikapu, Mbio, Mpira wa Pete, Tennis, na Badminton. Mashindano hayo yalimalizika rasmi tarehe 31 Agosti, 2014. Kwa ujumla shule Tanzania hazikufanya vyema, kutokana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na muda mfupi wa maandalizi