Taifa kwa sasa liko katika vuguvugu la
Matokeo Makubwa Sasa ikiwa ni msukumo wa Serikali ya Awamu ya Nne kuhakikisha
sekta zinazogusa maisha ya watu moja kwa moja mfano maji, afya, elimu,
usafirishaji na kilimo sinaangaliwa kwa jicho la pekee na Serikali.
Upande wa elimu, msukumo umewekwa
katika kuongeza udahili hasa wa wanafunzi wa sayansi ili kubabiliana na
upungufu wa wataalamu wa fani mbalimbali wa fani za sayansi.
Katika kuhakikisha hilo, jamii kupitia
asasi, mashirika ya dini, Serikali zinatakiwa kuweka msisitizo wa ujenzi wa
miundombinu yenye uwezo wa kuzalisha wahitimu wenye uwezo wa kupambana na
changamoto za kiutafiti, na kiutekelezaji katika fani hizo za sayansi
Lakini pamoja na utekelezaji wa mipango
na mikakati mingi ya kuhakikisha mafanikio yanapataikana, msingi imara katika
mafanikio hayo ni nidhamu.
Hilo limedhihirishwa na matoke ya
Kidato vidato vya Nne na Sita katika
shule zilizo chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, mathalani kwa shule zilizo
chini ya Jeshi la Kujenga Taifa; Jitegemee na Kawawa Sekondari. Matokeo ya
Shule yameonesha pamoja na kuwa na miundombinu na walimu wenye uwezo, dhana ya
nidhamu ni muhimu katika kufundisha na kujifinza.
Matokeo hayo ambayo Shule
ya Sekondari Kawawa (JKT) imefaulishwa kwa 100% na Jitegemee 97.2%
yamedhihirisha namna shule hizi zilivyodhamiria kuwa shule bora hapa nchini, na
kuwa tegemeo kwa Taifa.
Kwa upande wa Jitegemee (JKT)
Sekondari, mwanafunzi anapojiunga na shule anapitia mafunzo ya Kwata na kwa
ujumla ukakamavu. Mafunzo haya hutolewa kwa wanafunzi wapya wa Kidato cha
Kwanza na Tano na wahamiaji katika vidato vingine.
Mafunzo haya yamesaidia sasa wanafunzi kujenga utayari wa kujitunza
hasa katika utimamu wa mwili na akili, utayari wa kupokea maelekezo na maarifa katika ujifunzi, na kwa jumla
nidhamu ya kutambua wajibu wa kila mwanafunzi katika kutumia maarifa anayopata
kwa ajili yake, na jamii inayomzunguka.
Jitegemee na Kawawa sekondari zimekuwa
ni alama ya ufanisi wa Jeshi la Kujenga Taifa katika eneo la utoaji elimu bora.
Shule hizi zimekuwa na sifa ya pekee katika malezi na mafanikio ya wahitimu
wake baada ya kuhitimu masomo yao kwani wameajiriwa na kujiajiri katika
serikali kuu, sekta ya umma na binafsi.
Mfano Waheshimiwa Jerry Slaa (D)
Mstahiki Meya wa Ilala, Mhe. Lucy Mayenga Mkuu wa Wilaya, Mhe. Neema Mgaya
Mbunge; wasanii kama Marehemu Kanumba, Kajala, Temba (Mhe. Temba), Ras Pompi
Du, wacheza mpira maarufu kama Ally Mayai Tembele, Renatus Njohole (anayecheza
nje ya nchi) na wengine wengi waliohitimu Jitegemee.
Msingi wa mafanikio ni
nidhamu ambayo imesimamiwa vyema na Menejimenti ya Shule, walimu, wafanyakazi
wasio walimu, Serikali ya Wanafunzi, wanafunzi wenyewe na kwa ujumla mfumo bora
wa Jeshi la Kujenga Taifa, wa kuratibu na kusimamia utendaji na utekelezaji wa
majukumu kwa viongozi wote walio katika nafasi mbalimbali ndani ya Jeshi hilo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.