Friday, July 4, 2014

WACHEZAJI WA UJERUMANI WAKUMBWA NA UGONJWA

RIO DE JANEIRO (Ap) Wachezaji wa timu ya Taifa ya Ujerumani wamekumbwa na ugonjwa kabla ya mechi yao ya Robo Fainali na timu ya Taifa Ufaransa. Akiongea na vyombo vya habari, Kocha wa timu ya Ujerumani Joachim Loew alisema "theluthi moja ya kikosi chetu wamekuwa wakilalamika kuhusu kuwashwa koo" hii inafikiriwa ni kutokana na hali ya hewa. Alisema hata mchezaji beki wa kati Mats Hummels alishindwa kicheza mechi ya kufuzu na Aljeria, lakini akawa na matumaini atacheza katika Robo Fainali na Ufaransa.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.