
Mwalimu Joseph Modest Rutale aliyekuwa anafundisha masomo ya Hesabu na Fizikia katika Shule ya Jitegemee (JKT) Sekondari amefariki dunia kwa kujinyonga nyumbani kwake Ubungo Kibangu.
Habari zilizotolewa na mkewe Evodia Simon Lugeleka na baadaye kuthibitika kuwa kweli, mwalimu huyo alijinyonga siku ya Jumatano tarehe 23 Septemba 2009 asubuhi. Chanzo cha kujinyonga kwake hakijulikani kwani hakuacha ujumbe wowote. Mwalimu huyo pichani ameacha mke na watoto wawili Joel Joseph na Kelvin Joseph.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mwalimu Joseph Modest Rutale mahali pema peponi. Amina
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.