Shule ya Sekondari Jitegemee (JKT) imepata Bodi mpya ya shule baada ya ile iliyokuwapo kumaliza muda wake. Akizindua Bodi hiyo, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Maj Gen SN Kitundu ambaye kwa wadhifa wake ni Mwenye Shule, aliipongeza bodi iliyopita kwa kufanya kazi kwa bidii na kuiwezesha shule kuwa na mafanikio makubwa. Aliiasa bodi mpya kuendeleza yote mema yaliyofanywa na bodi hiyo na kuwa Makao Makuu ya JKT itakuwa bega kwa bega katika utekelezaji wa majukumu yake.
Alianisha maeneo ambayo bodi ya sasa itabidi kujielekeza nayo ni kuisimamia Menejimenti ya shule na kuishauri katika utekelezaji wa majukumu yake; kupitisha bajeti ya shule; kusimamia utoaji wa elimu bora kwa wasichana na wavulana bila ubaguzi (gender balance) na kuratibu matumizi bora ya rasilimali za shule.
Alihitimisha kwa kuwashauri kuunganisha nguvu za wadau wote wa elimu ili Jitegemee iendelee kuwa na mafanikio makubwa na kuaminiwa na jamii.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.