Friday, September 4, 2009
JITEGEMEE (JKT) SEKONDARI KUWA NA GAZETI
Hivi karibuni Shule ya Sekondari Jitegemee (JKT) inategemea kuzindua gazeti lake ambalo liko kwenye mchakato wa kusajiliwa liitwalo TEGEMEO LETU. Gazeti hilo litasheheni habari zinazohusu elimu kwa ujumla. Hii imetokana na ukweli kwamba elimu ni nguzo kuu ya mabadiliko ya maisha ya watu. Watu wakielimika ni rahisi kubadilisha maisha yao, mitazamo yao, fikra zao, mazoea yao, ufahamu wao, na kwa ujumla kuyafanya maisha yao yawe endelevu.
Elimu imekuwa tegemeo letu kijamii na ndio suluhu kuu ya mabadiliko ya uchumi, siasa, na kwa ujumla maisha yetu.
Kwa mfano tunapozungumzia umaskini, tunazungumzia kukosa uwezo wa kifikra, utashi, utaalamu, na mbinu za kuyabadilisha mazingira yetu yawe ya manufaa kwetu na hivyo umaskini wetu unaendelea.
Matatizo yanayoikabili jamii leo mengi yanatokana na kutokuwa na elimu inayoweza kutoa mwanga kwa jamii juu ya ni mambo yapi mema ya kutenda na yenye tija yanaweza kuibadilisha na kuipa mafanikio.
Jamii imebaki kubashiri njia muafaka ya kupata madhila yanayowapata ikiwa ni pamoja na kutafuta maendeleo. Ndio maana mauji kama ya albino, vikongwe, vichanga, walemavu wa viungo n.k. yamekithiri. Hii inatokana na jamii kukosa elimu sahihi ya namna ya kupambana umaskini ambao ndio chanzo kikuu cha watu kushindwa kumudu maisha.
Tegemeo Letu kwa hiyo linakuja kuleta ukombozi wa kweli dhidi ya licha ya changamoto kadha wa kadha ambazo zinaonekana mbele ikiwa ni pamoja na gharama za uendeshaji, uwepo wa magazeti mengi katika soko n.k. Lengo litakuwa ni kutoa habari za kweli, zinazohusu nini, nani, wapi, lini, na vipi (what, who, where, when, which, and how) matukio mbalimbali yanayohusu maendeleo ya elimu na changamoto mbalimbali zimejitokeza na namna ambavyo jamii inashiriki mchakato wa kupambana na changamoto hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.