Monday, March 1, 2010
KIDATO CHA SITA 2010 JITEGEMEE WAHITIMU
Tarehe 27 Januari 2010 ilikuwa siku njema kwa wanafunzi wote wa Kidato cha Sita mwaka 2010 kwani ndio siku waliyofanya sherehe ya mahafali ya 16 ya Kidato cha Sita.
Siku hiyo ilipambwa na hoihoi na nderemo kutoka kwa wahitimu, wazazi wa wahitimu, walimu pamoja na wafanyakazi wasio walimu, wageni waalikwa, na jumuiya yote ya Shule ya Sekondari Jitegemee (JKT).
Mgeni Rasmi katika sherehe hiyo alikuwa Ndugu Dustan Tido Mhando ambapo pamoja na mambo mengine aliwaasa wahitimu kujihadhari na maisha hatarishi kwani waendako ulimwengu umeharibika.
Akizungumzia dhana ya kufanya bidii katika masomo aliwaambia kuwa hakuna jambo muhimu la kuwapa watoto kwa sasa kuliko elimu. Elimu ndio ukombozi wa kwa kijana wa kizazi hiki hivyo lazima kila mmoja wao anatakiwa kuzingatia hilo.
Alisema ili kuleta maendeleo ya mtu na nchi kwa ujumla lazima kila mtu ajengewe uwezo wa kujitambua.
Awali Mkuu wa Shule Maj Martin Mkisi alielezea mafanikio makubwa ambayo shule imepata katika kipindi chote tangu ianzishwe. Alisema kuwa kwa sasa shule ina vifaa na miundo mbinu anuai zinazotumika katika kufundisha na kujifunzia kama vile maktaba, maabara, madarasa ya kisasa n.k.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.