Tuesday, October 20, 2009
WALIMU WA JITEGEMEE WAHUDHURIA MAFUNZO YA "MHAMO WA RWAZA"
Hivi karibu, walimu wa Shule ya Sekondari Jitegemee (JKT) walihudhuria mafunzo ya Mhamo wa Rwaza (Paradigm Shift) yanayoendeshwa na Taasisi ya Elimu (TIE) ambayo yanayosisitiza kumwezesha mwanafunzi kuonyesha namna ambavyo yale aliyojifunza yanamwezesha kuonyesha vipawa vyake mbalimbali (competence).
Mafunzo hayo yaliyofunguliwa na mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenerali Mwabulanga, yalianza tarehe 6 hadi 9 Oktoba 2009 kwa yeye kuwasisitiza walimu kuwa wasikivu na kuyafanyia kazi yote watakayojifunza.
Alisema "Dunia sasa imebadilika sana na hivyo elimu inayotolewa lazima iendane na mabadiliko hayo". Aliwakumbusha kuwa kizazi cha sasa kina vyanzo vingi vya taarifa kitu kinachowafanya wayajue mengi. Hivyo, mwalimu sio tena chanzo pekee cha maarifa kwa mtoto.
Wakati wa mafunzo hayo, walimu walijifunza tofauti iliyopo kati ya ufundishaji unaomtazama mwalimu kama chanzo cha maarifa "content based teaching" na ule unaomtazama mwanafunzi kama mdau katika kujifunza hivyo kuhitaji uwezeshaji "competence teaching and learning".
Wawezeshaji wa Mafunzo hayo Ndugu Stephen Mwinuka, Ms Dorothy Makunda, Ndugu Fredrick Mkebenzi, Ndugu Godson Lema, Ms Jane Kamwela na Ndugu Said Liguo walitumia mbinu mbalimbali ili kuwafanya walimu kujifunza na hii ilidhihirisha uwezo wa mfumo huu mpya kuwa unaweza kutoa mchango mzuri kwa wanafunzi kujifunza.
Akifunga Mafunzo hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Taasisi ya Elimu Tanzania Ndugu Kisanga aliusifu Uongozi wa Shule kwa kuwa miongoni mwa shule za awali kupokea mafunzo haya.
Alisema kusudi la kubadilisha mtaala au kufanya mapitio yake ni kuondoa mambo yaliyopitwa na wakati na kuingiza mapya kutokana na mahitaji ya wakati huo. Hivyo, mafunzo ya Mhamo wa Rwaza yamekuja kwa wakati ili kuendena na mahitaji ya sasa ambayo mwanafunzi anahitaji zaidi uwezeshaji kuliko kufundishwa. "Mafunzo haya yanamfanya mwanafunzi aonyeshe "competence" kitu ambacho kinamsaidia katika kujifunza" alisema. Aliwasifu walimu wote walioshiriki akasema ni matumaini ya wote kuwa sasa aina ya ufundishaji itabadilika na matokeo yake yatakuwa mazuri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.